Mwanamke wa Nigeria aweka rekodi mpya ya rekodi ya dunia ya Guinness kwa wigi refu zaidi

Mwanamke wa Nigeria ameweka rekodi ya dunia ya Guinness kwa kutengeneza wigi refu zaidi kutengenezwa kwa mkono.

Helen Williams alitengeneza wigi lenye urefu wa hadi  mita 351.28 (1,152ft 5”).

Mwanamke wa Nigeria aliyeweka rekodi mpya ya rekodi ya dunia ya Guinness kwa wigi refu zaidi

Alitumia siku 11 na milioni mbili (£2,000: $2,500)Naira 2,000,000 ambazo ni sawasawa na ksh 3,62839,  kuunda kipande cha nywele. Ilichukua bando 1,000 za nywele, makopo 12 ya dawa ya kupuliza nywele, mirija 35 ya gundi ya nywele na klipu za nywele 6,250.

“Mafanikio haya ni mojawapo ya mambo mazuri zaidi ambayo yamewahi kunitokea. Bado siwezi kuamini,” alisema.

Licha ya kuwa mtengeneza wig kwa miaka minane, alisema haikuwa kazi rahisi kwani “alihisi kuchoka” wakati wa mchakato huo.

“Marafiki na familia walinitia moyo. Sikutaka kuwaangusha, hivyo nilidumisha mtazamo wangu. Matokeo yake ni wigi refu zaidi lililotengenezwa kwa mkono duniani,” alisema.

Baada ya kukamilisha kipande cha nywele, ilikuwa vigumu kupata mahali pa kuitandika na kuipima kwa usahihi. Alichagua kuitandika kwenye barabara kuu inayounganisha miji ya Lagos na Abeokuta tarehe 7 Julai.

Rekodi za Dunia za Guinness zilithibitisha rekodi hiyo Jumanne.

Bi Williams ameonyesha wigi katika ofisi yake ili watu waweze kuja na kuangalia juhudi zake za kuweka rekodi.

Mapema mwaka huu, nchini Nigeria wengi wamejaribu kuweka rekodi mbalimbaliza dunia ikiwemo Hilda Baci aliyezua hisia nchini Nigeria alipovunja rekodi ya dunia ya kupika bila kukoma.

 

Leave a Reply