Mwanamume mwenye umri wa miaka 32 amefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa jaribio la kuua kufuatia madai ya kumdunga mpenzi wake kisu shingoni.
Mwanamme huyo David Njuguna akiwa amefikishwa mbele ya Hakimu Mwandamizi Gerald Mutiso wa Mahakama ya Makadara, alishtakiwa kwa kujaribu kumuua Mary Wangechi katika nyumba yao iliyoko Githurai 44 Estate.
Kwa mujibu wa jarida la Nairobi News liliripoti kwamba Njuguna pia alishtakiwa kwa kumjeruhi Wangechi kinyume cha sheria na kifungu cha 237 (a) cha kanuni ya adhabu.
Wangechi angali anapigania maisha yake katika Hospitali ya Thika Level 5.