Hali ya wasiwasi ilitanda kijiji cha Tian katika Kaunti ya Baringo baada ya mwanaume kumuua kwa kumchoma kisu mwalimu wa shule ya sekondari ya chini.

Picha ya mkanda wa eneo la uhalifu. Picha: Getty Images.
Chifu wa lokesheni ya Cheberen Sammy Kandie alithibitisha kisa hicho akisema mwanamume huyo aliyetambuliwa kama Kirwa kutoka Banita
kaunti ya Baringo alimvizia Leonida Tarus akiwa amejihami kwa kisu na kumdunga hadi kufa.
“Ni jambo la kusikitisha kwamba mwanaume huyo alimvizia mwanamke katika Shule ya Msingi ya Tian, akamdunga kisu hadi kufa na kisha akakimbia, lakini akapatikana amejinyonga kwenye mti jana. Ni jambo la kusikitisha kwa sababu shule nzima ilitegemea mwalimu huyo,” chifu wa eneo la Cheberen alisema.
Kulingana na chifu wa eneo hilo, uchunguzi ulionyesha wapenzi hao walikuwa na watoto wawili pamoja na awali walikuwa wanaishi pamoja hadi pale migogoro ilipoanza kujitokeza.Mapambano ya kuachana yaweza kuwa yalimfanya mwanaume achukue uamuzi wa kipekee, na mapenzi yalipoharibika, mwanamume huyo aliamua kumuua mwanamke huyo.
Chifu aliongeza kuwa wapenzi hao wanatoka Banita, Mogotio, Kaunti ya Baringo, na mwanamke husika alikuwa amehamia Cheberen ili kufundisha katika shule ya msingi ya Tian.