Mwili wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara Umepatikana Kichakana

Mwili wa mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara mwenye umri wa miaka 20 umegunduliwa ukiwa kwenye kichaka mita chache kutoka katika taasisi hiyo iliyoko Narok.

Kulingana na Shirika la Utangazaji la KBC liliripoti kuwa marehemu, aliyetambuliwa kama Adah Nyambura Ameru, aliripotiwa kutoweka Jumapili, Aprili 30, na mpenzi wake wa miaka 23, Brian Kimutai.

Picha ya mkanda wa eneo la uhalifu.

 

Nyambura aliripotiwa kutoweka Jumammosi usiku baada ya kuondoka kwenye klabu maarufu kama Elevate usiku katika mji wa Narok.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok John Kizito alisema mwili wa Nyambura ulipatikana ukiwa nusu uchi katika kichaka cha Macedonia na wananchi ambao walitoa taarifa kwa polisi.

Kizito alifichua kuwa mwili huo ulikuwa nusu uchi ukiwa na michubuko midogo usoni, na pia wanashuku kuwa marehemu alibakwa kabla ya kuuawa.Huku akitoa wito kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuzingatia masomo yao akisema michango yao inahitajika sana katika kuendeleza taifa.

“Taifa zima linasubiri kwa hamu huduma zenu. Tafadhali zingatia kufanya utafiti na chochote kitakachokuza taaluma yako ukiwa shuleni,” akashauri kamanda wa polisi.

Leave a Reply