Basi La Kampuni ya Climax Lapata Ajali mjini Migori

Basi la abiria kampuni ya Climax limehusika katika ajali asubuhi ya leo Mei 2,2023 Migori,Kenya .

Basi hilo la Climax Coaches lililo na maandishi ’THE DEVIL AWAY’ linalofanya safari zake Nairobi kwenda Sirare  limepata ajali baada ya dereva kushindwa kukata kona katika eneo la Kawa Mjini Migori.

Picha za Basi la Climax Lililop[ata ajali Migori

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo wanasema kwamba kulikuwa na majeruhi wengi ambao wote walipelekwa katika hospitali kuu ya Kaunti Ya Migori.

Picha za Ajali iliyotokea Migori

Picha za ajali ya hiyo gari la Climax

Hii imetokea ikiwa ni wiki tatu tu zimepita baada ya ajali mbaya ya lori iliyoua zaidi ya watu 10 mjini Migori.

Tutazidi kukujuza habari zaidi kuhusiana na ajali hii.

Leave a Reply