Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia kwa ajali leo April 25, 2023.
Watatu hao wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wanasafiria aina ya Noah kwenda kwenye shughuli ya mahafali ya kijana wao aliyehitimu kidato cha sita.
Ajali hiyo ilitokea mkoani Kilimanjaro baada ya Noah hiyo kusombwa na mafuriko katika Kata ya Malula Tarafa ya King’ori Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Picha kutoka eneo la Ajali Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akiwa katika eneo la tukio amesema katika ajali hiyo miili ya Watu watatu (Wanawake wawili na Mwanaume mmoja) imepatikana, na mwili unaosadikiwa kuwa wa mtoto bado unaendelea kutafutwa.