Mwanamke wa asili ya Kihindi, 75, Auawa na Wafanyikazi Wake Nyumbani Kwake Kisumu,kenya.

Polisi wanawasaka washukiwa wawili, mwanamume na mwanamke, wanaoaminika kumuua mwajiri wao Mhindi mwenye umri wa miaka 75 katika Mji wa Kisumu nchini Kenya.

Katika tukio hilo, wawili hao wanatuhumiwa kumkosesha hewa na kumnyonga mwanamke huyo hadi kufa nyumbani kwake eneo la Milimani.

Akithibitisha kisa hicho, Naibu Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kisumu ya Kati Jackton Mango alisema wawili hao walimtuma mlinzi wa nyumba hiyo kununua mboga ili kutekeleza uhalifu huo.

Kisha walimfunga mkongwe huyo miguu na mikono kabla ya kumuua. Nia ya wawili hao kuangamiza maisha ya mwajiri wao bado haikujajulikana.

Inaripotiwa kuwa mshukiwa huyo wa kiume alikuwa amemtumikia marehemu kwa miaka 8 huku mwanamke huyo akiwa na miezi minne tu katika nyumba hiyo.

Hivyo inasadikika unyama huo ulifanyika katika chumba chake cha kulala kwani ndiko mwili wake ulipatikana ukiwa na alama za kunyongwa.

Leave a Reply