Amuua Kakake wa Damu kwa Kisu wakigombea Chakula

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24 anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Siaya kwa tuhuma za kumuua kakake katika kijiji cha Sirongo-Oware kaunti ya Siaya nchini Kenya.

 

Kwa mujibu wa chifu wa kata ndogo ya Kakumu-Kombewa Philip Ogola, mwendazake alikuwa anaanda chajio mshukiwa alipowasili na kutoa amri ya kupewa chakula.

Mshukiwa,Lawrence Oduor Wayodi kwanza alimmwagia maji kakake,Erick Otieno mwenye umri wa miaka 26 akitaka chakula kabla ya ugomvi kuzuka na vita kuanza kabla ya kuchukua kisu na kumdunga hadi kufa.

Ndugu hao mayatima walikuwa wakiishi katika boma la wazazi wao.

Baada ya kutekeleza kisa hicho, Oduor alijiwasilisha katika ofisi ya naibu chifu kupiga ripoti kuwa alikuwa amemuua kaka yake.

Naibu Chifu anasema kuwa alitembelea eneo la tukio na kupata mwili wa Otieno ukiwa umelala katika kidimbwi cha damu na majeraha ya kisu kifuani.

Hivyo Naibu Chifu alipiga ripoti katika kituo cha Polisi ambapo polisi walipeleka mwili huo katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Rufaa ya Siaya na mshukiwa kutupwa seli.

 

Leave a Reply