Aliyekuwa Waziri wa Elimu Prof George Magoha alifariki Jumanne, Januari 24.

Aliyekuwa Waziri wa Elimu Prof George Magoha alifariki Jumanne, Januari 24.

Magoha mwenye umri wa miaka 71 alikata roho katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa akipatiwa matibabu. Kulingana na mawasiliano rasmi kutoka kituo hicho, Magoha alianguka nyumbani kwake kabla ya kukimbizwa huko.

 

Huku familia yake ikiweka wazi kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali hiyo James Nyamongo alithibitisha kifo hicho na kueleza kuwa Magoha alikata roho muda mfupi baada ya kufika katika kituo hicho.

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunatangaza kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha Prof George Magoha jioni hii katika Hospitali ya Nairobi.

“Magoha alianguka nyumbani na kukimbizwa hospitali katika chumba cha  Ajali na Dharura. Juhudi za kumfufua hazikufua dafu. Tafadhali ungana nami kuwapa pole familia yake,” Nyamongo alitangaza.

Magoha ameacha mke wake Dkt Barbra Magoha na mwanawe Dkt Michael Magoha.

Kifo chake kinakuja wiki moja tu baada ya kuteuliwa kama mhadhiri wa upasuaji wa kimatibabu katika Shule ya Udaktari ya Chuo Kikuu cha Maseno.

Mara ya mwisho Magoha kuonekana hadharani ni pale alipokabidhi majukumu ya Wizara ya Elimu kwa mrithi wake, Ezekiel Machogu.

Leave a Reply