Wanawake watatu wapigwa na radi hadi kufa Vihiga

Wanawake watatu kutoka Lwanda,kaunti ya Vihiga wamepigwa na radhi hadi kufa .

Mvua kubwa ilikuwa inanyesha hivyo wanawake hao walikuwa kwenye kibanda kando ya barabara wakati tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili jioni.

Picha: Hisani

Hata hivyo, watu kadhaa waliofika eneo la tukio walisema wawili kati yao ni wauza ndizi katika mji wa Luanda na wa tatu ni msichana mwenye umri wa makamo.

OCPD wa eneo la Luanda, David Ndirangu alithibitisha kisa hicho na kusema alifahamishwa kuhusu suala hilo.

“Nimefahamishwa na mamlaka ya eneo hilo kwamba watu watatu wameuawa na radi wakati wa mvua ya jioni hii,” Ndirangu alisema Jumapili jioni.

“Ni bahati mbaya kwamba wanawake hao watatu walikuwa wamechukua kivuli kwenye kioski kando ya barabara,” aliongeza.

Miili yao ilikuwa imelala kando ya barabara nyuma ya Hoteli ya Triple T katika kaunti ndogo ya Luanda kabla ya kuchukuliwa na maafisa.

Leave a Reply