BABA MTAKATIFU MSTAAFU BENEDIKTO XVI AFARIKI DUNIA

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI (95) amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 31,2022 majira ya saa tatu na dakika 34 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook wa Vatican News ujumbe unasomeka:

“With sorrow I inform you that the Pope Emeritus, Benedict XVI, passed away today at 9:34 in the Mater Ecclesiae Monastery in the Vatican. Further information will be provided as soon as possible.”

(Kwa masikitiko ninawataarifu kwamba Papa Mstaafu Benedict XVI amefariki dunia leo saa 9:34 katika Monasteri ya Mater Ecclesiae mjini Vatican. Taarifa zaidi zitatolewa haraka iwezekanavyo).

Picha ya Baba Mtakatifu Benedict XVI

Papa wa zamani Benedict XVI amefariki dunia katika makazi yake Vatican, akiwa na umri wa miaka 95, karibu muongo mmoja baada ya kujiuzulu kwa sababu za kiafya.

Tarehe 16 Aprili 2022, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliadhimisha Kumbukizi ya Miaka 95 tangu alipozaliwa.

Tangu mwaka 2013 amekuwa akiishi kwenye Hosteli Mater Ecclesiae iliyoko ndani ya Bustani za Vatican.

Papa Benedict aliongoza Kanisa Katoliki kwa muda usiozidi miaka minane hadi mwaka 2013, akawa Papa wa kwanza kujiuzulu tangu Gregory XII mnamo mwaka 1415.

Mrithi wake Papa Francis alisema alikuwa anamtembelea huko mara kwa mara. Licha ya kwamba papa huyo wa zamani alikuwa mgonjwa kwa muda, Baraza Kuu lilisema kumekuwa na hali mbaya katika hali yake kwa sababu ya uzee.

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake Jumatano tarehe 28 Desemba 2022 kuhusu Sherehe ya Noeli, Mwaliko kwa waamini kutafakari pamoja na Wasalesian wa Don Bosco, Mama Kanisa anapoanza kuadhimisha Jubilei ya Miaka 400 tangu Mtakatifu Francisko wa Sales, Askofu, Mwalimu wa Kanisa na Msimamizi wa Waandishi wa Habari alipofariki dunia tarehe 28 Desemba 1622, amewaalika kwa namna ya pekee kabisa, waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kusali na kumwombea Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ambaye alisema alikuwa mgonjwa sana.

Leave a Reply