Amuua kakake baada ya kupigana, kugombania dada yao waliokuwa na uhusiano wa kimapenzi nae

Maafisa wa Upelelezi wanamsaka mwanamume wa umri wa miaka 31 ambaye anadaiwa kumuua kakake mkubwa katika kisa cha madai ya ugomvi wa kimapenzi unaohusisha dada yao mdogo katika eneo la Kirinyaga nchini Kenya.

Inasemekana mshukiwa alimpiga kakake mwenye umri wa miaka 37 kwa kutumia kifaa butu kichwani, usoni na mgongoni baada ya kumpata katika mazingira ya kutatanisha na dada yao wa kambo mwenye umri wa miaka 17. 

Idara ya DCI ilisema kwamba ndugu hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na dada yao mwenye umri wa miaka 17.

“Marehemu pia alikuwa na mapenzi ya siri na msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 na hakuweza kukubaliana na kile alichokishuhudia,” taarifa hiyo ilisema. 

Marehemu aliaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Karatina. 

Maafisa wa Upelelezi waliofika katika eneo la mkasa waligundua kuwa marehemu awali alikuwa amedaiwa kumpa ujauzito dada yao mwaka jana, lakini alipoteza ujauzito huo mwezi Machi mwaka huu.

Leave a Reply