Watumiaji wa WhatsApp watafurahia vipengele sita vipya baada ya Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa Facebook, Mark Zuckerberg, kutangaza mabadiliko hayo mapya Alhamisi, Novemba 3.
Vipengele vilivyokusudiwa kuboresha ubora wa mwingiliano wa kikundi (Group) ndani ya jukwaa ni pamoja na;

Kura
Kura za maoni ni njia ya kufurahisha na shirikishi ya kushirikiana na watu kwa kuwauliza maoni yao. Wanakikundi sasa wanaweza kufanya na kushiriki katika kura kwenye gumzo.
Uwezo wa kutumika kwa viungo vya simu(Links)
Wanakikundi sasa wanaweza kuunda na kushiriki viungo vya kupiga simu na marafiki na familia kwa ajili ya mkutano ulioratibiwa. Unaweza kufanya hivyo kwa kwenda kwenye kichupo cha kupiga simu, ambapo utapata aikoni ya ‘unda kiungo cha simu’, ambayo itazalisha kiungo ambacho unaweza kushiriki na mtu yeyote.
Jumuiya /Communities
Jumuiya zitaboresha vikundi kwa kuwezesha vikundi vidogo na kupanga soga zao kuhusu mambo wanayopenda au kushiriki.
Kipengele hiki kimewekwa kando ya kichupo cha gumzo, hali/status na kile cha kupiga au kupokea simu.
“Pamoja na jumuiya/Communities, wasimamizi sasa watakuwa na na uwezo wa kupanga mazungumzo sehemu moja.”
Majibu ya kikundi
Watumiaji wa kikundi sasa wanaweza kujibu au kuitikia (react) soga za kikundi na maudhui yanayotumwa kwa kikundi kwa emoji kwa kubofya picha au gumzo. Kabla ya hili, watumiaji wangeweza tu kuitikia kwa picha na gumzo katika mazungumzo ya kibinafsi.
Wito wa watu hadi 32 kwa pamoja
Watumiaji sasa wanaweza kupiga simu na hadi watu 31 kwa wakati mmoja, ambayo inapita kikomo cha awali cha watu 8.
Kutuma au kupokea faili kubwa
Sasa mtu anaweza kutuma au kupokea hadi uzito wa GB 1.9 ya faili na watu unaowasiliana nao. Kabla ya utambulisho huu, watumiaji wangeweza kushiriki faili zisizozidi MB 100 pekee.
Mkurugenzi Mtendaji alitaja kuwa utambulisho huo ulichochewa na nia yake ya kukuza mwingiliano salama wa familia wa karibu wenye umoja.
“Ninaamini kuwa familia zilizounganishwa zinahitaji njia za kibinafsi na salama za kuunganishwa ndani yao wenyewe.”
Hii inafuatia viongezo vya hivi majuzi vya programu, kama kubofya aikoni ya wasifu wa mwasiliani ili kuona statasi yake.