Vibes and Benali live yawapa vijana jukwaa la kutangaza talanta zao.

 

Kenya ni kitovu cha vipaji, jambo ambalo halina mjadala.

Mamilioni ya vijana wa Kenya wamebarikiwa kuwa na vipaji mbalimbali kuanzia muziki, kandanda, uigizaji, na kucheza dansi, riadha, miongoni mwa vingine.

Hata hivyo, ni wachache waliobahatika kupenya na kuwa watu waliotaka kuwa kutokana na ukosefu wa majukwaa ya kuonyesha vipaji vyao.

Mtayarishaji wa muziki na Mhandisi wa sauti Benali alianza na kufanya mahojiano ya moja kwa moja na wanadada. Baada ya kugundua kuwa wanadada wengi  wanakuwa wananyanyaswa na walinzi wa lango la tasnia, kila siku ikawa hakuna wanawake wanaoinuka katika tasnia ya Kenya. Aligubikwa na wingu jeusi kuskia hayo hivyo akaamua kuacha mahojiano hayo na kutafuta suluhisho ambalo ni kuunda jukwaa la kuinua vipaji.

Picha ya Benali Jukwaani akizindua Vibes na Benali Live Picha: Hisani ya Benali

Mhandisi huyo ambaye ameona na kufanya mengi mazuri kwenye tasnia ya muziki na vipindi vya runinga alizindua rasmi kipindi chake kilichopewa jina la ‘Vibes and Benali Live’  Februari mwaka huu.

Katika maonyesho mara mbili tangu Vibes and laughs kuzinduliwa mashabiki wa tasnia wamejitokeza kwa wingi kuwapa sapoti zaidi ya vipaji 20 ambao wamebahatika kuonyesha talanta zao kwenye jukwaa hili.

Mashabiki katika Onyesho la Vibes na Benali Live Picha;Hisani ya Benali

Akizungumza na Trifam Media, Benali ameweka wazi kuwa mikakati na mipangilio ya mwaka 2023 ni kuhakikisha maonyesho haya yanapeperushwa kwenye runinga za humu nchini. Na pia ameishukuru kampuni ya Across solutions ambayo imekuwa ya msaada sana kuona maono hayo yanafanikiwa.

‘’Kwa sasa hivi,kuna mikakati na mipangilio ya kuweka kwenye televisheni…. hivyo tukiingia 2023  ndio contracts za TV zitakuwa……na nashukuru Across solutions wamekuwa wakinisupoti sana kuhakikisha haya maono yanaendelea.’’ Benali alisema.

Kama kazi nyingine ile, kuzindua Vibes and Benali Live haijakosa kuwa na changamoto ila macho yake ameyaelekeza kwa kuwa mabadiliko yanayostahili ili kuweza kuwawezesha vijana. Hivyo, yeye na team yake wanawahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya majaribio watakapo kwenda kwenye kaunti mbalimbali kubadilisha tasnia nzima kuwa bora na kuzindua taaluma mpya.

Tofauti na maonyesho mengine ya kawaida, ambayo hubainisha talanta fulani yaani vichekesho, kuimba, hili litakuwa wazi kwa talanta zote kimsingi chochote ambacho kiko chini ya sanaa ya ubunifu.

Vijana wakionyesha talanta zao kwenye jukwaa la Vibes na Benali Live.

Pia amewataka mashabiki kumfuatilia kwenye mitandao yake ya kijamii (Benali Ke) kwa kuwa ataweka wazi zaidi kuhusu onyesho la Vibes and Benali Live litakalofanyika Desemba 17 mwaka huu ambayo pia ni siku yake ya kuzaliwa.

Leave a Reply