Ndege mbili za Kijeshi zimegongana angani na kulipuka huko Dallas, Texas Marekani.

Ndege hizo zilikuwa zikishiriki kwenye maonesho ya WWII maarifu kama siku ya maveterani ambapo inahofiwa huenda watu wote waliokuwemo ndani yake wakawa wamefariki kutokana na ndege hizo kuanguka na kuwaka moto.
Ripoti ya maafisa wa jeshi la anga wanaweza kuwa ndege yenye Chapa ya B-17 kulikuwa na jumla ya watu 6 ndani huku ndege yenye Chapa P-63 ikiwa na watu 5 ambao wote hali zao bado hazijawekwa wazi.
Ndege hizo ni Boeing B-17 iliyotengenezwa mwaka 1930 nchini Marekani huku ya pili ikiwa ni Bell P-63 ambayo matoleo yake yalitengenezwa nchini humo kati ya mwaka 1943-1945.