Mswada wa ukomo wa mihula miwili kwa rais kuwasilishwa bungeni hivi karibuni.

Mbunge wa Fafi Salah Yakub amefichua kuwa mipango ya baadhi ya washirika wa Rais William Ruto inaendelea kurekebisha Katiba.

Mbunge wa Fafi Salah Yakub

Yakub anadai kuwa sehemu hiyo ya wabunge wa United Democratic Alliance (UDA) wanapanga kubadilisha ukomo wa mihula miwili ya urais na badala yake ukomo wa umri wa miaka 75. Yakub alifichua haya kwa mara ya kwanza katika harakati ya kusambaza chakula cha msaada huko Garissa mwishoni mwa juma.

“Tunataka kuwaambia Wakenya kwamba kikomo cha mihula miwili kinafaa kubadilishwa. Tunataka kibadilishwe hadi kikomo cha umri ambapo mtu akifika miaka 75 basi hawezi kugombea,” alisema.

Mbunge huyo wa UDA aliongeza: “Tutakuja na Mswada wa marekebisho ili kujaribu kubadili hili kwa sababu tunataka sharti liwe na ukomo wa umri na si masharti, ikiwa rais anafanya kazi nzuri basi hatakiwi kuwekewa mipaka na sheria au masharti.”

Pia alifichua kuwa wapendekezaji hao bado hawajatayarisha mswada wa marekebisho ambao utawasilishwa Bungeni.

Kitu ambacho kimepingwa vikali na viongozi mbalimbali nchini ikiwemo mwenyekiti wa chama cha Uda,Johnson Muthama na Boni Khalwale.

Johnson Muthama: Tafadhali zingatia hili; kama Mwenyekiti wa Chama Taifa, naomba niseme wazi kwamba Mhe. Yakub ametoa taarifa binafsi ambayo haina uhusiano wowote na UDA. Kama Chama, tunasimamia Demokrasia iliyo wazi, na tunasalia kuunga mkono ukomo wa urais wa mihula miwili na hakuna majadiliano yanayoendelea ya kuufuta.

Boni Khalwale: Mhe Salah Yakub, Mbunge mpya wa Eneobunge la Fafi. Sijamfahamu bado. Ni kweli kwamba anafurahia uhuru wa kusema.

Hata hivyo, lazima akumbushwe kwamba UDA inaamini katika fundisho la Muundo wa Msingi & Vifungu muhimu katika Katiba yetu. Amekosea na yuko nje ya utaratibu kabisa.

One Response

  1. Makorre Wilson November 8, 2022

Leave a Reply