Mhubiri Amnajisi kisha kumuua Mtoto wa Miaka 10  

Polisi katika eneo la Rangwe katika Kaunti ya Homa Bay wanamsaka mhubiri anayetuhumiwa kumnajisi na kumnyonga mtoto wa miaka 10 siku ya Alhamisi,3 jioni.Vitendo vilivyomsababishia kifo mtoto huyo.

Picha ya mtu aliyevalia aina ya vazi linalovaliwa na wahubiri wa Legio Maria.

Ripoti ya polisi inasema kuwa mwanamume huyo anaripotiwa kumfuata msichana huyo nje, akamshambulia na kumnyonga katika shamba la mahindi na kumwacha na maumivu makali.

Mpita njia alitokea na kupiga kamsa ambapo msichana huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay, lakini alifariki dunia alipokuwa akipokea matibabu.

Kwa mujibu wa waliomuona mwanaume huyo kabla ya kutoweka walisema mwanamume huyo alikuwa amevalia kanzu ambayo mara nyingi huvaliwa na waumini wa Legion Maria alikuwa katika nyumba ya kina mtoto huyo kwa maombi.

Jamaa za mtoto Vivian Akoth, wanasema alikutana na mshukiwa wakati alipokuwa ametumwa nyumbani kwa bibi yake kuchukua kibuyu cha kuteka maji.

Nyanya yake alimtambulisha mwanamume huyo kwa jina moja tu Abraham ambaye alisema alikuwa mgeni wake kutoka Kisumu.

Afisa wa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Kaunti hiyo ndogo Monica Berege alisema wamemkamata mwanamke mzee ambaye anasemekana alikuwa na mshukiwa wakati tukio hilo lilitokea.

“Anaweza tu kumtambua mshukiwa kwa jina moja. Lakini alikuwa akifanya nini na mwanaume huyo nyumbani kwake ikiwa hamjui? Tunafanya kila tuwezalo kumkamata mshukiwa mkuu,” Berege alisema.  

Leave a Reply