Mama akamatwa na Polisi  kwa kuwachoma moto watoto wawili

Polisi Mkoa wa Njombe nchini Tanzania wanamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kuwachoma watoto wake wawili na kuwasababishia madhara makubwa.

Mafiga

Akizungumza na wanahabari mkoani Njombe Kamanda wa Polisi, Hamis Issah amesema mwanamke huyo Adelina Ngollo (36) anadaiwa kuwachoma watoto hao ambao mmoja ana umri wa miaka (4) na mwingine (7) kutokana na tabia yao ya kwenda kwa majirani na kuombaomba chakula.

“Kitendo alichokifanya mama huyu akikubaliki kabisa akidai sababu ya kuwachoma moto hawa watoto hakuwa makini kuwaangalia kwani watoto walikuwa wanatembea tembea kwa majirani na kuomba chochote kitu ili wajikimu na siku iende,” amesema Issah.

Amesema baada watoto hao kuwa na tabia hiyo majirani walimuita mwanamke huyo na kumueleza kuwa malezi ya watoto hao siyo mazuri, maneno hayo yalimuumiza na kuyaweka moyoni.

Kamanda Issah ameeleza kuwa mwanamke huyo alipofika nyumbani kwake aliwaamsha watoto wake wawili na kuwachoma moto kwa kutumia jiko la mafiga matatu linalotumia kuni na kuungua mikononi na sehemu zingine za mwili.

Amewataka wananchi mkoani Njombe kuwalea watoto katika misingi mizuri.

Leave a Reply