Jamaa Amteka Nyara Mwanawe kisha kuitisha 50k kutoka kwa mkewe.

Makachero wa DCI wamemkamata jamaa mmoja kutoka eneo la Embakasi Nairobi Kenya ambaye alimteka nyara mwanawe na kisha kudai kitita cha pesa kabla ya kumwachilia.

Aliyemteka nyara mtoto wake kisha kudai alipwe na mke wake

Inaripotiwa walikuwa na ugomvi na mkewe na ndipo akaamua kumteka nyara mtoto huyo wa miaka minane na kumwambia mkewe amtumie pesa hizo.

DCI walisema alimchukua mtoto huyo nyumbani na akajihami na kisu huku akimwandikia mkewe ujumbe kuwa alipe 50,000Ksh au angemthuru mtoto.

  “Mara tu mama huyo alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Embakasi, makachero kutoka kikosi cha uhalifu waliitwa na kupangwa, walianza kumsaka mshukiwa mara moja,” DCI walisema kwenye twitter.

Makachero walifaulu kumpata na kumshika mshukiwa alipokuwa amejituliza akisubiri mkewe kumtumia fedha alizokuwa ameitisha.

Kwa sasa mshukiwa huyo ameshikilishwa katika kituo cha polisi cha Embakasi akisubiri kushtakiwa huku mkewe na mwanawe wakiendelea na maisha yao kama kawaida.

Leave a Reply