Amuua Mwanamke kwa kumkata kata kisha kuchoma mwili wake na kula kama mshikaki

 

Mwanaume mmoja anashikiliwa na Polisi katika eneo la Kaloleni wilayani Songwe nchini Tanzania kwa kumuua mwanamke,kuukata kata mwili wake na kuuchoma moto kisha kuula kama mshikaki.


Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya hiyo Simon Simalenga ni kuwa Usiku wa Novemba 13, 2022, mwanaume huyo Lazaro Adamson (40) anadaiwa kumuua Berta Shugha (69)  kwa kumpiga panga kisogoni na katikati ya kichwa na kwamba alipopoteza maisha ndipo akaanza kumkata kata.

“Alisema baada ya kumuua alimkata nyayo za miguu yote, akatoa utumbo na kuukamulia kwenye beseni na yeye anadai kuwa alianza kula kwa vile alikuwa na hamu ya nyama,” amesema DC Simalenga.

Awali baadhi ya viungo vya marehemu havikujulikana vilipo na baadaye vilipatikana

“Baadhi ya viungo ambavyo vilikuwa havionekani kama vile mapaja, hatimaye Askari wetu wa Jeshi la Polisi wamevipata vikiwa vimefichwa katika shimo la choo ambacho kilikuwa hakitumiki, viungo hivyo vimepatikana vikiwa vimechomwa na katika hali ya kushangaza mtuhumiwa alianza kula nyama hiyo mbele ya Askari,” ameongeza Simalenga.

Wakizungumzia tukio hilo,baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Chang’ombe walisema walishtukia uwepo wa mauaji hayo baada ya kuona damu nyingi zikiwa zimezagaa kwenye nyumba ya mtuhumiwa, jambo ambalo halikuwa la kawaida.

Leave a Reply