Zaidi ya watu 132 waripotiwa kufariki baada ya daraja la watembea miguu kuanguka nchini India

Watu zaidi ya 132 wamefariki dunia baada ya daraja linalotumiwa na waenda kwa miguu kuvunjika katika jimbo la magharibi la Gujarat nchini India.

Kulingana na  maafisa wa eneo hilo, wengi wa wale waliofariki ni wanawake, watoto na wakongwe. Daraja hilo lililoko katika mji wa Mobi, lilifunguliwa rasmi juma moja lililopita baada ya kufanyiwa ukarabati.

Daraja lililoporomoka India

Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya daraja hilo kufunguliwa tena, kufuatia ukarabati uliokuwa ukifanywa.

Daraja hilo lililojengwa toka enzi za ukoloni katika karne ya 19, wakati wa utawala Uingereza lina urefu wa mita 230 na ni maarufu kama kivutio cha utalii katika eneo hilo.

Mmoja ya watu aliyeshuhudia ajali hiyo anasema kulikuwa na watoto wengi katika daraja hilo la wenda kwa miguu, wakati lilipokatika.

 Bado chanzo cha kuvujika kwa ajali hiyo hazijafahamika, lakini mamlaka za Enei hilo zinasemamsongamano wa watu katika daraja hilo wakati huu wa msimu wa sikukukuu ya diwali inaweza pia kuwa sababu.

Gujarat ni nyumbani kwa waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ambaye ametangaza kuwa familia za waathiriwa zitafidiwa.

Leave a Reply