Wafuasi wa Ruto wapata ajali wakielekea Kasarani

Wafuasi wa Rais Mteule William Ruto kutoka kijijini Sugoi wamepata mkosi walipokuwa wakielekea Kasarani kushuhudia mtoto wao akiapishwa.

Picha Za Ajali

Watu 31 walipata majeraha mabaya baada ya basi la shule lililokuwa wakitumia kupoteza mwelekeo, kubingiria mara kadhaa na kuingia kwenye mtaro katika eneo la Sachangwan barabara ya Eldoret- Nakuru. 

Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya kaunti ya Molo kwa matibabu huku safari yao ya kushuhudia Ruto akiapishwa ikikatizwa.

Shughuli zinaendelea kushika kasi katika uwanja wa Kasarani ambapo takriban wafuasi 60, 000 wamefika kushuhudia William Ruto akiinua Biblia.

Ruto anatarajiwa kuchukua hatamu za uongozi rasmi hivi leo ambapo shughuli hiyo ya kuapishwa tayari inaendelea katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani ambapo pia itakuwa siku ambapo rais anayeondoka Uhuru Kenyatta ataanza maisha tena kama raia.

Tayari takribani viongozi 20 wa mataifa ya Afrika na wageni 2500 spesheli wamefika kwenye sherehe hiyo.

Rais Uhuru anatarajiwa kumkabidhi Ruto upanga wa uongozi kama ishara kwamba sasa ndiye Amirijeshi Mkuu.

Hata hivyo, kulingana na aliyekuwa mpinzani mkuu wa Ruto, Raila Odinga, hajafika na hatafia Kasarani.

Hii ni licha ya kualikwa na Ruto kupitia barua na hata simu aliyopigiwa Jumatatu jioni.

“Leo jioni nimepokea simu kutoka kwa Dr William Ruto akinialika kwa sherehe ya kuapishwa kwake itakayofanyika hapo kesho. Nasikitika kuwa sitaweza kuhudhuria sherehe hiyo kwa sababu niko nje ya nchi na pia kwa sababu zingine,” alisema kwenye taarifa hapo jana.

Leave a Reply