Vikao vya kwanza vya Bunge la kitaifa na Seneti na uapisho.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza Alhamisi, Septemba 8 kama tarehe ya kwanza ya vikao vya Seneti na Bunge la Kitaifa.

Siku ambayo pia Wabunge wa Bunge la Kitaifa na seneti wataapishwa.

Rais Uhuru Kenyatta

Zoezi hilo litafanyika siku ya kwanza kwa Bunge la 13 litafanyika katika mabunge hayo mawili kuanzia saa tatu asubuhi.

“Mimi, Uhuru Kenyatta, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Ulinzi wa Kenya, ninateua kwamba Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Kitaifa na Seneti utafanyika katika Majengo makuu ya Bunge,” alisema kwenye Notisi ya Gazeti Nambari 10527.

Katika Bunge la kitaifa kutakuwa na wajumbe 349 wakiwemo Wawakilishi Wanawake 47 na Wabunge 12 wa Kuteuliwa. La Seneti, kwa upande mwingine, itakuwa na wanachama 67, wakiwemo Maseneta 20 Waliopendekezwa.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Kenya Rais anatakiwa kutangaza tarehe ya kikao cha kwanza cha Bunge jipya kupitia notisi ya gazeti la serikali ndani ya siku 30 baada ya uchaguzi.

Leave a Reply