Mwanaume Mashuhuri Instagram Apigwa Risasi na Kufa.

Mwanamume ambaye amekuwa akionyesha maisha ya kifahari kwenye mitandao ya kijamii alipigwa risasi na kufa huku maelezo yakibainika kuwa alikuwa mhalifu sugu.

Source: Prince’s Instagram profile

Mwanaume huyo mrembo kutoka Afrika Kusini aliyetambulika kama Prince ‘Mongol’ Mahlangu aliuawa kwa kupigwa risasi na mshambulizi asiyejulikana huko Pretoria.

Kulingana na ripoti, kigogo huyo wa Instagram alipigwa risasi na mshambuliaji aliyekuwa akiendesha gari nyeupe aina ya VW Polo. Mshukiwa alikabiliana na mwathiriwa na baada ya kuzungumza, alimpiga risasi kadhaa kabla ya kukimbia kwa kasi.

Prince alikuwa pamoja na mke wake wakati mshambuliaji alimpiga.

Kwa bahati nzuri, mkewe alinusurika katika shambulio hilo la kikatili.

Ingawa alidai kuwa mfanyabiashara kwenye mitandao ya kijamii, maelezo sasa yanaibuka kuwa alikuwa sehemu ya kikundi cha uhalifu kilichohusika na wizi wa magari na wizi wa benki.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotumwa kwenye mtandao wa twiter zinaonyesha kuwa mnamo Februari 2022, Prince anadaiwa kuwa sehemu ya kundi la wahalifu waliomuua mlinzi wa G4S kwa kumpiga risasi na bunduki aina ya R5 alipokuwa akipakia pesa kwenye lori la kampuni hiyo.

2 Comments

  1. Wycliff Omondi September 8, 2022

Leave a Reply