Malkia Elizabeth wa pili aliendelea kuombolezwa baada ya kifo chake wiki jana.
Mwili wa malkia huyo wa muda mrefu wa Uingereza wiki hii ulilazwa katika eneo la Westminster kwa umma kutoa heshima za mwisho kwake huku walinzi wakiwa wanaulinda usiku na mchana.
Katika video moja ambayo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonekana mlinzi mmoja akipoteza fahamu na kuanguka chini huku umati ukiwa unazidi kupanga foleni kuutazama mwili wa Malkia Elizabeth.
“Wanajeshi waliandamana na jeneza kutoka Buckingham Palace siku ya Jumatano lakini mmoja wa walinzi katika Ukumbi wa Westminster dhiki ilionekana kuwa nyingi sana kwani alizimia ghafla. Kulikuwa na miguno kutoka kwa waombolezaji alipokuwa akianguka chini ambayo ilinaswa kwenye video. Ilitokea wakati kundi la walinzi wakianza kubadilishana majukumu na mmoja alionekana kutetemeka kabla ya sekunde chache kuanguka,” jarida la Mirror nchini Uingereza liliripoti.
Maafisa wawili wa polisi walionekana wakikimbia kumchukua kabla ya video kukatwa na kisha kwenda kwenye picha za Mabunge.
Tazama video hiyo hapa: