Amason Kingi achaguliwa kuwa Spika wa Seneti ya Kenya.

Aliyekuwa gavana wa Kilifi Amason Kingi ndiye spika wa seneti ya Kenya baada ya kujizolea jumla ya kura 46.

Speaker Amason Kingi

Kingi alichaguliwa katika awamu ya kwanza kwa kuafikia kigezo cha thuluthi mbili (kura 45) ya jumla ya maseneta au kura 67.

Hata hivyo alipata kura 46 kati ya 67 katika awamu ya kwanza na ya mwisho ya upigaji kura. 

Kingi sasa anachukuwa nafasi ya Ken Lusaka ambaye ni gavana wa Bungoma.

Shughuli ya upigaji kura na kuapishwa kwa Kingi iliongozwa na katibu wa seneti Jeremiah Nyegenye. 

Mapema muungano wa Azimio ulipata pigo baada ya mgombea wake Kalonzo Musyoka kujiondoa kutoka kinyang’anyiro hicho.

Hatua hiyo ya Kalonzo iliyotangazwa na katibu wa Seneti Jeremiah Nyegenye ilimpiga jeki Kingi katika kujizolea kura nyingi.

Nyegenye alisema kwamba ofisi yake ilikuwa imepokea barua asubuhi siku ya Alhamisi kutoka kwa Kalonzo akiondoa azma yake.

Maseneta katika muungano wa Azimio siku ya Jumatano walikuwa wameafikia kwa kauli moja kumuunga mkono Kalonzo kwa wadhifa wa Spika wa seneti.

Hivyo Speaker Amason Kingi atapata mshahara wa shilingi Milioni1,160,000 kila mwezi.

Leave a Reply