Huduma ya mkopo ya Fuliza imepunguza ada zake za kila siku kwenye mkopo kwa asilimia 40.
Siku ya Jumatano huduma ya Safaricom na benki za NCBA na KCB zilitangaza punguzo ya ada, ambayo kulingana na kampuni hizo ni hatua ambayo itasaidia ukuaji wa matumizi ya huduma za mkopo.

“Wateja wa Fuliza watafurahia matengenezo ya kila siku bila malipo kwa siku tatu za kwanza, baada ya kukopa pesa, kwa miamala ya chini ya Sh1,000,” Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa alisema.
Ndegwa alisema mabadiliko hayo yataathiri asilimia 80 ya miamala iliyofanyika, akieleza kuwa idadi hiyo ni uthibitisho kuwa Fuliza inafikia lengo lake.
Ada mpya itaanza kutumika tarehe 1 Oktoba 2022.
Akizungumza Jumatano wakati wa mkutano uliofanyika ili kurekebisha Fuliza.
Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi waliohuduria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Norfolk jijini Nairobi.
“… tunapunguza ada ya kila siku kwa asilimia 50 kwa miamala ya Fuliza ya Sh1,000 na chini,” alisema.
Ndegwa aliongeza kuwa pia kutakuwa na makato katika ada ya kila siku kwa miamala inayozidi Sh1,000 hadi Sh70,000.
Alisema ada ya ufikiaji wa Fuliza itadumishwa kwa asilimia moja ya sasa katika shughuli zote na mabadiliko hayo yanasababisha makato ya jumla ya asilimia 50 ya ushuru wa Fuliza.
“Hii inathibitisha Fuliza kama njia ya mikopo inayofikika zaidi na nafuu kwa asilimia moja tu ya thamani ya muamala, hasa wateja wanapolipa ndani ya muda mfupi,” Ndengwa aliongeza.
Rais William Ruto alikuwepo wakati wa mkutano huo.
Alisema ada ya ufikiaji wa Fuliza itadumishwa kwa asilimia moja ya sasa katika shughuli zote.