Raila Odinga Apinga Matokeo ya Urais Yaliyotangazwa Jana na IEBC

Mgombea Urais kwa tiketi ya Azimio la Umoja Raila Odinga ameongea na vyombo vya habari akiwa katika jumba la KICC jijini Nairobi.

Mgombea wa Urais Raila Odinga akiongea na wanahabari KICC

Hii ni kwa mara ya kwanza baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kutangaza Mshindi wa Urais kuwa ni William Ruto hapo jana.Odinga amemkashfu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Wafula Chebukati, kuwa alitumia nguvu na kutangaza matokeo ya Urais yasiyo ya kweli.

“…nawashukuru Wakenya wenzangu walioshiriki uchaguzi, nawashukuru Wafuasi wa AZIMIO kwa kutofanya fujo au kujichukulia hatua mkononi baada ya matokeo kutangazwa na ninawaomba waendelee kuwa watulivu….Hivyo hatukubali  matokeo hayo na tutafuata sheria ili kupata haki ya demokrasia….

” amesema Odinga.

“Sisi tunapenda amani, tunapenda umoja wa wakenya…Tuko na nia ya kutaka kuona ya kwamba kenya imetoka katika janga la ufukara,kutokuwa na imani,amani…. hatutakubali mtu mmoja ajaribu kuleta vurugu… na kubadilisha vilevile yale yaliyoamuliwa na Wakenya…..Mungu ibariki Kenya Nchi yetu…..”  amesema Raila Odinga.

Pia Odinga amewaomba wakenya kuwa watulivu na kuzingatia amani.

Leave a Reply