Wanakandarasi wa tume ya uchaguzi IEBC wakamatwa Katika uwanja wa Ndege na Kuachiwa huru baada ya siku.

Abiria  wa kigeni ambaye Alhamisi alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) akiwa na stika za uchaguzi za IEBC ameachiliwa kutoka kizuizini.

Kulingana na Msemaji wa Polisi nchini Kenya Bwana Bruno Shioso, siku ya Alhamisi abiria alinaswa akiwa na roli 17 za stika za majimbo mbalimbali ya uchaguzi nchini. Stika ambazo hazikuandamana na afisa wa IEBC ilivyo utaratibu wa kawaida kwa mujibu wa Sheria.

Msemaji wa Polisi Kenya,Bruno Shioso

“Polisi, kulingana na utaratibu na mpangilio wa kawaida na IEBC, hawakuarifiwa kuhusu uagizaji kama huo mapema ili kutoa usalama muhimu na kusindikiza,” akaongeza.

Hivyo mshukiwa na stika hizo ambazo zilikuwa kwenye begi lake la kusafiria alizuiliwa na kupelekwa katika makao makuu ya DCI ambako maafisa wa upelelezi walianza uchunguzi wao, polisi walitaka kuelewa kwa nini abiria alikuwa amebeba stika hizo na ni nani aliyempa.

Abiria huyo aliachiliwa baadaye na stika kukabidhiwa IEBC baada ya  uchunguzi kumebaini kuwa stika zilizopatikana ni mali ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

“Kukamatwa, kuzuiliwa  kwake ni kwa sababu ya kumiliki  vifaa vya uchunguzi ” alisema.

Huku Tume ya uchaguzi , IEBC, ikieleza kusikitishwa kwake kutokana na hatua ya serikali kuwakamata wanakandarasi wake watatu, wanaohusika na maandalizi ya uchaguzi wa mwezi ujao.

Taarifa kutoka IEBC, imesema watatu hao wafanyakazi wa kampuni ya Smartmatic International BV, walikamatwa punde baada ya kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, wakitokea nchini Venezuela.

IEBC imesema kukamatwa kwa watatu hao hakuna msingi wowote na kwamba wanakandarasi hao walisafiri hadi Kenya kuhakikisha mitambo ya electroniki itakayotumiwa kwenye uchaguzi mwezi ujao, inafanya kazi bila matatizo, IEBC ikisema ilikuwa imetoa taarifa kwa vyombo vya usalama kuhusiana na ujio wa wanakandarasi hao.

Hata hivyo idara ya polisi mapema Ijumaa imetoa taarifa na kusema watatu hao wameachiliwa huru baada ya uchunguzi kukamilika.

Kenya inajianda kwa uchaguzi wa tarehe 9 mwezi ujao.

3 Comments

  1. Makorre Wilson July 22, 2022
  2. Makorre Wilson July 22, 2022

Leave a Reply