Mashindano ya Kombe la EURO kwa wanawake kuanza England

Mashindano ya kombe la EURO 2021 kwa wanawake yanatarajiwa leo Jumatano (06.07.2022) England. Mechi ya ufunguzi itakuwa ni kati ya wenyeji England, The Lioness, na Austria.

    Mechi ya ufunguzi inachezwa Jumatano (06.07.2021) kati ya England The Lioness na Austria katika uwanja wa Old Trafford na fainali itachezwa uwanjani Wembley Julai 31. Mechi ya ufunguzi itavunja rekodi ya mashabiki 41,000 kujitokeza uwanjani kutazama mechi, kwa zaidi ya mashabiki 30,000, katika mashindano ya EURO, huku mashabiki karibu 90,000 wakitarajiwa kuwa uwanjani kutazama fainali huko Wembley.

Takriban tiketi milioni moja zimeshauzwa kwa mashabiki katika nchi 100 kote ulimwenguni, huku tiketi zote za mechi ya leo ya ufunguzi zikiwa zimenunuliwa zote.

Huku wenyeji England chini ya kocha Mholanzi Sarina Wiegman, ambaye aliiongoza Uholanzi kushinda kombe la EURO mwaka 2017, wakiwa wametolewa nje ya mashindano ya EURO katika nafasi ya nusu fainali.Safari hii wanakabiliwa na kibarua kigumu kuhakikisha wanafikia matarajio ya mashabiki wao washinde taji la kwanza la mashindano makubwa katika udongo wa nyumbani.

 Uzoefu wa Kocha Wiegman unatarajiwa kuwasaidia England kupata matokeo mazuri. Kocha Wiegman amesema kikosi chake kiko katika fomu nzuri sana. Hajashindwa katika mechi 14 kama kocha wa England tangu alipochukua mikoba Septemba mwaka uliopita.

    

One Response

Leave a Reply