Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 26 mkazi wa Manushi Wilayani Moshi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mkubwa pamoja na mkewe kwa kuwacharanga na panga kutoka na tuhuma za kuwa wanamroga.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa alisema tukio hilo limetokea Julai 19 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika Kijiji cha Manushi kati.
Kamanda Maigwa, alisema kuwa awali kabla ya tukio hilo mtuhumiwa Jonas Mushi alifika nyumbani kwa marehemu na kuingia ndani na kuchukua panga na kuanza kumshambulia baba yake mkubwa aitwae Mariki Mushi.
Wakati akiendelea kumshambulia ndipo mke wa marehemu aitwae Felista Mushi alipoingilia kwa lengo la kumsaidia mumewe asishambuliwe ndipo mtuhumiwa alimgeukia mama yake mkubwa na kuanza kumshambulia.
Aliongeza kuwa, chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina kwani mtuhumiwa anawatuhumu marehemu kuwa ni wachawi na wamekuwa wakimroga.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.
Dunia ina mambo kweli