Mawakala Bandia wa Freemason wakamatwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania linawashikilia watu 23 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya utapeli kwa njia ya mtandao.

Kwa ushirikiano wa timu maalumu ya Kuzuia na Kupambana na Uhalifu wa Mtandaoni na jeshi hilo,operesheni hiyo ya kati ya Mei 18 hadi Juni 26 ilifanyika pia katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro ambapo watuhumiwa wengine walikamatwa huko.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Jumanne Muliro

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema waliokamatwa ni  watuhumiwa waliokuwa wakijifanya wakuu wa shule, waganga wa kienyeji, ndugu wa waathirika, wahudumu wa makampuni ya simu au mawakala wa Freemason.

Amesema watuhumiwa hao huwatumia watu ujumbe mbalimbali kupitia namba tofauti za simu na kujifanya wanania ya kusaidia watu badala yake huishia kuwaibia.

Waliokamatwa ni Julius Simon Mwabula (20) ambaye ni mkazi wa Ifakara Morogoro sambamba na wenzake 22.

Watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na vifaa mbalimbali ambavyo wanavitumia kufanya uhalifu huo ikiwemo  simu za aina tofauti 28, kompyuta ya mezani 1, flash 2, Kompyuta mpakato 2,  modem ya mitandao yote na kadi za simu za mitandao mbalimbali zaidi ya 50.

2 Comments

  1. Elpinah June 28, 2022

Leave a Reply