IEBC Kuchapisha sajili ya mwisho ya Wapiga kura Jumanne

Wafula Chebukati

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Jumanne Juni 21, inatarajiwa kuchapisha notisi ya gazeti la serikali kuhusu sajili ya mwisho ya wapigakura itakayotumiwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu matokeo ya ukaguzi wa KPMG, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema jumla ya wapoga kura 22,120,458 wamesajiliwa kushiriki uchaguzi katika vituo 46,232 kote nchini.

Chebukati alifutilia mbali utumizi wa sajili ya wapiga kura kwa mikono katika uchaguzi huo akisema vituo vya kupigia kura visivyo na mtandao vitatumiwa na modem za satelaiti kusambaza matokeo.

Leave a Reply