Waandishi Wa Habari Wapigwa Mawe   “Yanarushwa Na Mizimu”

Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali Mkoani Arusha wametimuliwa kwa kupigwa na mawe ambayo hayajulikani yanapotokea katika kijiji cha Kiwawa Kata ya Imbasei Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Inaelezwa kuwa katika hali isiyo ya kawaida waandishi hao wamekumbana na hayo baada ya kufika kwenye eneo hilo kwa lengo la kufuatilia taharuki ya wananchi kupigwa kwa mawe yanayohisiwa kurushwa na Mizimu.

Mwandishi mmoja wa GADI TV amejeruhiwa sehemu ya kichwani kwa kupigwa na jiwe huku mwandishi mwingine wa GLOBAL TV akijeruhiwa mkono wake wa kushoto.

Leave a Reply