Rais wa Guinea Bissau avunja bunge, aitisha uchaguzi

Rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo amelivunja bunge na serikali ya nchi hiyo na kusema kuwa utaitishwa uchaguzi wa mapema mwaka huu ili kutatua mzozo wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu.

Rais wa Guinea Bissau

Kulingana na amri mbili za rais, Waziri Mkuu Nuno Gomes Nabiam na naibu wake Soares Sambú wataendelea na nyadhifa zao na watahakikisha utendakazi wa watendaji hadi uchaguzi utakapokamilika.

Mvutano kati ya bunge na urais umelikumba taifa hilo la Afrika magharibi kwa miezi kadhaa. Embalo alitaja tofauti zinazoendelea na zi-sizoweza kutatuliwa na bunge, ambazo alielezea nafasi ya siasa za msituni na njama.

Kwa mujibu wa katiba uchaguzi utafanyika ndani ya siku 90 ila amri ya Rais ilisema uchaguzi wa bunge utafanyika Disemba 18.

Baada ya kuvunjwa, tume yake ya kudumu inachukua majukumu ya bunge hadi uchaguzi ufanyike.

Leave a Reply