Raila Amtaja Mgombea Mwenza huku Kalonzo akijitoa kwenye Muungano wa Azimio

Mgombea urais wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga hatimaye amemteuwa kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua kuwa mgombea mwenza.

Mgombea Urais ,Raila Odinga na Martha Karua

Akimtaja kwenye hafla iliyofanyika nje ya Jumba la Kimataifa la Mikutano (KICC),Raila alisema kwamba Jopo la Azimio la Kuteuwa Mgombea Mwenza lilitoa ripoti na kusema Karua aliibuka bora kwa nafasi hiyo.

Jopo hilo pia lilikuwa limewahoji magavana Charity Ngilu (Kitui), Hassan Joho (Mombasa), Lee Kinyanjui (Nakuru) na Wycliffe Oparanya (Kakamega) ,kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua kuwania nafasi ya mgombea mwenza wiki jana

Wengine waliohojiwa ni Mwakilishi wa Kike wa Murang’a Sabina Chege, Waziri wa Kilimo Peter Munya na aliyekuwa Mbunge wa Emgwen Stephen Tarus.

Huku hayo yakijiri Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amegura muungano wa Azimio na kutangaza kuwa atakuwa kwenye  kinyang’anyiro cha Urais cha Agosti 9 kwa tikiti ya OKA.

Akizungumza katika makazi yake makuu ya Karen Kalonzo ametaja kutokuwa na imani katika muungano wa Azimio kama kikwazo cha kugura muungano huo.

“Kama hamna imani, huwezi fanya biashara,kwa muda gani tutajitolea hata baada ya kujitolea wanaharibu,” Kalonzi Alisema.

Pia amemteua mwanasiasa Andrew Sunkuli kuwa mgombea mwenza wake.

Leave a Reply