Mwalimu wa Madrasa mbaroni kwa kuwalawiti wanafunzi zaidi ya 20.

Mwanamme mmoja ambaye ni mwalimu wa Madrasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani wa Arusha kwa tuhuma za kuwalawiti wanafunzi zaidi ya 20 wa shule ya msingi Mkonoo katika jiji la Arusha.


Tukio hili limeibuliwa na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda baada ya kufika katika shule hiyo na kuzungumza na wazazi, walimu na wanafunzi baada ya kukamilisha alichoita uchunguzi wake juu ya mwalimu huyo wa madrasa.

Mwanaume mbaroni

Amesema Mwalimu huyo Jumanne Ikungi  wa madrasa amekuwa akiwarubuni kwa pipi, miwa na zawadi nyingine watoto hao na kuwafanyia ukatili ambao Serikali haiwezi kuvumilia.


“Nimeagiza wanafunzi waendelee kufanyiwa uchunguzi katika hospitali na madrasa kufungwa na mtuhumiwa kuendelea kushikiliwa na polisi  hadi hapo uchunguzi utakapokamilika,” amesema.


Mtanda akiwa katika shule hiyo iliyopo pembezoni mwa jiji la Arusha ameagiza wanafunzi wote kuandika upya kama wamefanyiwa matukio yoyote ya ukatili na baadae Serikali itafanya uchunguzi zaidi.


Awali Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mkonoo, Lucian Monino amesema walianza Kubaini uwepo wa matukio ya uhalifu baina ya wanafunzi na Mzee Jumanne anayeishi jirani na shule baada ya utoro kuongezeka shuleni.


Jeshi la polisi mkoa Arusha limekiri kumshikilia Jumanne Ikungi na uchunguzi ukikamilika atafikishwa Mahakamani.

One Response

  1. Wilson May 20, 2022

Leave a Reply