Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky amemtunuku tuzo ya heshima ya Rais mbwa aliyepewa jina Pattern kwa huduma zake tangu uvamivi wa Urusi.

Mbwa huyo mdogo kiumbo na mwenye umri wa miaka miwili na nusu amekuwa shujaa wa kitaifa nchini Ukraine, ishara ya upinzani wa Ukraine dhidi ya Urusi.
Mbali na kubaini marundo zaidi ya 200 ya nyaya zinazohusishwa na vilipuzi, mwezi April alitajwa kugundua mabomu zaidi ya 90. Mbwa huyo amekuwa maarufu chini ya kitengo cha usalama tangu uvamizi wa Urusi.
“Ninataka kuwatunuku mashujaa hawa wa Kiukreni ambao tayari wanasafisha ardhi yetu, mbwa huyu sio tu anasaidia kubaini vilipuzi, lakini pia hufundisha watoto wetu kanuni muhimu za usalama katika maeneo ambayo kuna hatari”
Sherehe ya tuzo hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, ambaye aliwasili Ukraine siku ya Jumapili, Justin Trudeau alitangaza kwamba Canada itatoa silaha zaidi na vifaa kwa Ukraine.
Rais Zelensky alikabidhi medali kwa mbwa huyo na mmiliki wake My Hello Ilyo.