Mwanamume mmoja amefariki baada ya kujinyonga katika kanisa moja huko Kenol, Kaunti ya Murang’a nchini Kenya.
Mwili wa John Maingi, 35, ulikutwa ukining’inia kwenye paa la Kanisa la Remnants of Church Fellowship, siku ya Jumatano baada ya kujitia kitanzi.
Kwa mujibu wa Polisi, mchungaji katika kanisa hilo alikuwa akifungua jengo hilo alipogundua kuwa lilikuwa limefungwa kutoka ndani. Baada ya kusaidiwa na wananchi kufungua, waligundua mwili huo ukining’inia ndani.
Marehemu alikuwa ametumia kitambaa cha meza kujitoa uhai. Mwili ulitolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Tukio hilo linachunguzwa na polisi.
Labda huyu aliamini kufa ndani ya kanisa kutampatia tiketi ya mbinguni. Pole kwa familia yake
Kweli,kila na mtu na fikira zake.