‘Mtasubiri Sana’  Video ya Wimbo Wa Diamond Platinumz Ft Zuchu Yafungiwa kuchezwa kwenye vyombo vyote vya utangazaji.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa Diamond Platnumz ft. Zuchu “mtasubiri sana” kutokana na kipande kinachoonesha Zuchu akiwa Kanisani kwenye kwaya kisha kuacha kuimba na kupokea simu.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na TCRA imesema “kipande hicho cha video kimeleta ukakasi miongoni mwa Waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kwamba ni dharau juu ya dini/madhehebu fulani hivyo kwa barua hii TCRA inaagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii hapa nchini kutorusha video ya wimbo huo hadi hapo Msanii tajwa (Diamond Platnumz) atakaporekebisha sehemu hiyo ya video”

Video hiyo ya Diamond Platnumz ft. Zuchu iliachiwa March 29 2022 kwenye mtandao wa Youtube na mpaka sasa ina views milioni kumi na laki tatu elfu kumi na sita mia tano na saba.

Leave a Reply