MSANII wa Bongofleva, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari, usiku wa kuamkia leo, April 14, 2022.

Kwa mujibu wa Banana Zorro ambaye ni kaka wa marehemu, mdogo wake alifariki kufuatia ajali ya gari iliyotokea saa chache baada ya kuachana nae. Taarifa hiyo ambayo Banana ameiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kuwa gari alilokuwa akiendesha Maunda liligongana na lori la mchanga na kusababisha umauti wake.
Aidha Banana ameeleza kuwa aliachana na Maunda saa 12 jioni baada ya kujumuika kwenye msiba wa rafiki yao wa muda mrefu. Saa nne usiku baada ya kuachana nae alipata taarifa za ajali na kifo cha mwanamuziki huyo kutoka kwenye familia ya mwanamuziki Zahir Ally Zorro.
Msanii Maunda aliwahi kutikisa kwenye bongofleva kupitia nyimbo zake kadhaa ikiwemo ‘Nataka niwe wako’ na Mapenzi ni ya wawili.
Maunda ameacha watoto watatu.
Pole kwa familia yake na wamamuziki Kwa jumla, hili ni pigo kubwa!!
Kwa kweli haya maisha mafupi mno.