Mfungwa Mwanamke awapachika mimba wanawake wawili

Wafungwa wawili katika gereza la wanawake pekee wamepata ujauzito baada ya kulala na mfungwa aliyebadili jinsia. Mfungwa aliyebadilisha jinsia.

Wanawake hao ni miongoni mwa watu 800, wakiwemo wanawake 27 waliobadili jinsia wanaozuiliwa katika Kituo cha Marekebisho cha Edna Mahan huko Clinton, New Jersey.

Katika barua iliyotumwa kwa vyombo vya habari, mfungwa mmoja alidai kuwa mmoja wa wanawake hao alikuwa na ujauzito wa miezi mitano.

Ripoti hiyo ilisema kuwa wafungwa hao walikuwa na historia ya vitendo vya ngono katika maeneo ya umma na ilibidi watenganishwe.

Kupitia tovuti ya Justice 4 Demi, anayoiendesha akiwa gerezani, Minor aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 akiwa na umri wa miaka 16 kwa kuua bila kukusudia amekiri kuwa ndiye aliwapa mimba wafungwa hao wawili .

Kwa sasa ameidhinishwa kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha tabia.

 Mwanamke anayedai kuwa mama wa mmoja wa watoto hao ameandika chapisho la blogi kwenye tovuti hiyo, linaloitwa ‘Uhuru, Upendo, Mimba na Kiwewe’. “Cha kushangaza nina ujauzito wa miezi mitatu na nilijifungua nikiwa nimefungwa hapa Edna Mahan Correctional Facility,” aliandika.

Leave a Reply