Mahakama moja mashariki mwa Rwanda imemhukumu Imam Muislamu kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuua nguruwe msikitini.
waraka wa mahakama hiyo unasema kwamba Sadate Musengimana alikubali kumuua nguruwe huyo ‘kwa bahati mbaya’ mwezi Februari alipofika karibu na msikiti na kuvuruga mafundisho yake ya quran.
Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa watoto walipopiga kelele kwa kuona nguruwe msikitini, Bw Musengimana alitoka nje ili kumfukuza kwa fimbo, alimpiga na akafa, lakini hakuwa na nia ya kumuua.
Upande wa mashtaka ulikuwa umeomba kifungo cha miaka saba jela dhidi ya Bw Musengimana, huku utetezi wake haukuona sababu yoyote ya kifungo cha miaka mitano jela ikiwa ni mara moja zaidi kupatikana na hatia ya kuua mnyama wa kufugwa kwa nia mbaya katika sheria za Rwanda.
Raia wa Rwanda kwenye mitandao ya kijamii na vikundi mbalimbali wameonyesha mshtuko kujua hatima ya Bw Musengimana ilipotoka kwenye vyombo vya habari.
Hata hivyo Wakili wake Bw. Yusuf Nsengiyumva amesema Musengimana yuko gerezani tangu Februari 2022 alipomuua nguruwe huyo huku akilaani hukumu kali kutolewa kwani mteja wake alimuua nguruwe huyo kwa bahati mbaya.Hivyo wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
Nchi na sheria zake,
Duuuh