Waliofanya KCPE Mwezi Wa Tatu 2022 Kujua Matokeo Yao Leo.

Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane mwaka 2021 watafahamu matokeo leo.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha wiki jana alitangaza kuwa shughuli ya usahihishaji ilikuwa imekamilika na matokeo yangetangazwa rasmi leo Jumatatu au Jumanne.

Matokeo hayo yatatolewa kwa umma rasmi baada ya kukabidhiwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na hilo litategemea na ratiba ya Rais.

Mtihani wa KCPE ulifanyika kati ya Machi tarehe 7 na 9 2022 ambapo watahiniwa 1,225,507 walifanya mtihani wa KCPE mwaka 2021, kulinganisha na 1,191,752 wa mwaka 2020.

Hata hivyo waliofanya mtihani huo wanatarajiwa kuanza kujiunga na kidato cha nne mwezi Mei. Mtihani huu ulichelewa kufuatia kuathirika kwa kalenda ya masomo kutokana na janga la korona.

Bonyeza link ifuatayo kujua jinsi ya kuangalia matokeo hayo yatakapotangazwa.

One Response

  1. Binti March 28, 2022

Leave a Reply