Bado Niko ‘Ngangari’ Katika Injili Josee Blessed Atangaza Katika Wimbo Wake Mpya

Kwa hakika Josee Blessed amewabariki mashabiki wake kwa wimbo mpya wa injili Ngangari wimbo wa Kiswahili ambao anakanusha uvumi kwamba yeye si mkristo tena. Wimbo kwa jina Ngangari ambao pia ni wa kwanza kuachiwa mwaka 2022 kutoka kwake baada ya kuachia wimbo unaoitwa corona mwaka mmoja uliopita.

Wimbo Ngangari uliwaachiwa tarehe 22 mwezi wa tatu 2022.

Josee Blessed ambaye kabla ya kuachia wimbo huo alipokea simu na meseji nyingi mno kutoka kwa wapenzi wa mziki wake wakiwa na maswali mengi ni kwa nini amekimya au ameacha injili.Kitu ambacho kilimshangaza sana kwani wengine walikuwa na dhana kuwa ameishiwa na kutoka kwenye injili.Hivyo akaona ni vyema kuwapa jibu kupitia kwa wimbo huu aliouandika kwa umahiri.

Ngangari kwa Kiswahili humaanisha kuwa thabiti, na ni hapa ambapo Josee anaweka msingi wa ujumbe wa huo wimbo wake mpya wa injili unaovuma. Amewarai mashabiki kuweza kuuskiza wimbo huo Ngangari ili kuweza kupata majibu yote kumhusu yeye na ukimya wake.

Huu hapa chini..

Tazama wimbo Ngangari wa Josee Blessed kisha acha comment.

Leave a Reply