Watu 137 wameshauawa na 306 wamejeruhiwa katika kipindi cha chini ya masaa 24 yaliyopita nchini ikiwa ni siku ya kwanza tu ya shambulio la Urusi nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema hayo mapema leo Ijumaa.
Pia amelalamika kuwa nchi za Magharibi za Ulaya na Marekani zimejitenga nao katika kukabiliana na Russia huku akitoa mwito kwa wananchi wake kujilinda wenyewe na wasitarajie msaada wa kijeshi kutoka nchi za Magharibi.
Jana Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilisema kuwa, imeamua kuanzisha operesheni maalumu ya kijeshi nchini Ukraine ili kuzuia kutokea vita vikubwa vya dunia.
Akizungumza na televisheni ya “Rusia 24,” Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, lengo la nchi yake si kuliangamiza jeshi la Ukraine bali ni kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo na kuhakikisha kuwa usalama wa Russia unalindwa kwa kuyazuia madola ya Magharibi na NATO kukusanya majeshi yao katika mipaka ya Russia.
The NATO countries have failed Ukraine.