SERIKALI imetoa Sh3.2 bilioni kufadhili ujenzi wa madarasa ya Mtaala Mpya wa Masomo (CBC) kote nchini.

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha alisema fedha hizo zitatumwa moja kwa moja kwenye akaunti za M-Pesa za wanakandarasi kama njia ya kuhakikisha uwazi katika mchakato mzima.

“Hili ni onyo kwa baadhi ya maafisa wa Wizara ya Elimu ambao huenda wakataka kuweka vikwazo kuwa watachukuliwa hatua kali,” alisema Waziri Magoha baada ya kuzindua rasmi darasa moja katika shule ya St Cecilia Aluor Girls eneo la

Gem, Kaunti ya Siaya, Alisema kuwa madarasa karibu 1,000 yaliyojengwa kupitia mpango wa kuendeleza miundomsingi uliozinduliwa mnamo Oktoba 2021 tayari yamekamilishwa. Mradi huo ulianzishwa na serikali ili kuunda nafasi kwa wanafunzi watakaojiunga na sekondari za chini Januari 2023.

Pia akizindua madarasa mengine katika shule ya msingi ya Bungoma, Waziri wa Elimu, George Magoha amewaonya walimu wakuu dhidi ya kuwatimua wanafunzi shule hasa watahiniwa kwa sababu ya kukosa karo nakuongeza kuwa watakao patikana wana hatari ya kukamatwa.

3 Comments

  1. J HABUBA KE February 12, 2022
  2. Kovulo February 13, 2022
  3. Kovulo February 13, 2022

Leave a Reply