Polisi aua Mwenzake na kujeruhi mkuu wake 

Afisa mmoja wa polisi amuua mwenzake kwa mpiga risasi na kumjeruhi mkuu wake katika kambi moja ya polisi kaunti ya Meru nchini Kenya.

Chumba anatuhumiwa kumpiga risasi kichwani na kumuua afisa Pontianas Ikumoli, 22 kisha kutorokea kusikojulikana na bunduki yake ikiwa na risasi zisizopungua 17.

Afisa aliyejeruhiwa alipata jeraha katika mkono wa kushoto na alikimbizwa katika hospitali moja eneo hilo na kulazwa huko. Ambaye kwa sasa yuko katika hali nzuri.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walisema walikusanya risasi 13 zilizotumika na juhudi za kumsaka mshukiwa huyo bado zinaendelea.

One Response

  1. Kovulo February 23, 2022

Leave a Reply