Mwanamume mmoja kutoka Busia nchini Kenya anasemekana kupagawa baada ya kutambua kuwa mke wake anatoka kimapenzi na pasta au mchungaji wa kanisa.
Mwanaume huyo anayejulikana kwa jina Onyango mwenye umri wa Kati, ameteketeza nyumba yake baada ya kugundua kuhusu uzinzi huo na kisha baadaye mwili wake ulipatikana kando ya mto Busia.
Mwili wake ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Busia kufanyiwa upasuaji wa maiti ili kubaini kilichomuua huku familia yake ikiamini kuwa alijitoa uhai.
Kwa mujibu wa ripoti ya kituo cha runinga cha NTV, Onyango aliteketeza nyumba yake hiyo na baadaye mwili wake kupatikana kando ya Mto Busia.
Mwili wake umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Busia kufanyiwa upasuaji wa maiti huku familia yake ikiamini kuwa alijitoa uhai.
Ni furaha kupata habari kwa lugha ya kiswahili. Yanisanifisha kilugha. Asante