Mwanamume akamatwa kwa kuwanajisi mabinti wake watatu kwa miaka 3, na kuwapa magonjwa ya zinaa.

Mwanamume mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa Ijumaa kwa madai ya kuwanajisi binti zake watatu kwa muda wa miaka mitatu huko Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya.

Kulingana na Polisi, mshukiwa, alianza kuwanajisi wasichana hao baada ya kutengana na mkewe mnamo 2019.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Gichugu, Anthony Mbogo alisema kuwa suala hilo lilijidhihirisha baada ya watoto hao kumjulisha mwalimu wao wa shule ambaye aliwafahamisha maafisa wa kituo cha polisi cha Kianyaga.

Maafisa wa Ulinzi wa Mtoto wa eneo hilo walianza uchunguzi haraka na baadaye wakamkamata baba huyo, ambaye inasemekana alikiri makosa yake.

Watoto hao kwa sasa wako chini ya uangalizi wa Afisa wa Ulinzi wa Mtoto wa eneo hilo, huku mshukiwa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kianyaga akisubiri kufikishwa mahakamani ambapo atafunguliwa mashtaka ya unajisi.

Leave a Reply